Burudani

Ukiwa msanii ni lazima uwe na thamani yako ili kuogopeka – Country Boy

Msanii wa muziki Bongo, Country Boy amesema msanii ni lazima ajitengezee mazingira ya upekee kwa sababu hiyo ndio biashara yake.

Rapper huyo amesema kitu hicho kimemfanya baadhi ya wasanii kuogopa kufanya naye ngoma kutokana na kiwango ambacho amekiweka katika muziki wake.

“Ukiwa msanii ni lazima uwe na value yako, usiwe tu wa kawaida, hiyo ndio biashara siku zote. Navyojiweka na mazingira ambayo nimetengeneza ni mazuri na kunifanya niweze kuogopeka hata ukija unakuja na kazi bora,” Country Boy ameiambia Bongo5.

“Hata muziki wangu nauchukulia serious zaidi, kila ninachokifanya lazima ni kiogope na nikiheshimu, sijichukulii poa,” amesisitiza.

Country Boy kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Mwaaa’ aliyoshirikiana na Moni ambapo kwa pamoja wanaunda kundi la MoCo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents