Habari

Ulichaguliwa na Mungu kututambua Wanyonge – Mgunduzi wa Tanzanite kwa Rais Magufuli

Mtanzania aliyegundua madini ya Tanzanite, Mzee Jumanne Mhero Ngoma amesema kuwa Rais Magufuli alichaguliwa na Mungu kwa ajili ya kutetea wanyonge.

Kauli hiyo anakuja mara baada ya Rais Magufuli kumtambua rasmi kama mgunduzi wa madini hayo leo April 06, 2018.

“Asante kwa kunitambua kuwa ni mimi nilifanya shughuli hii hapa Mirerani, watu wote hawa wanashiba kwa ajili ya jamsho la mkono wangu,” amesema.

“Mhe. Rais inaeleweka wewe ulichaguliwa na Mwenyenzi Mungu ili uje hapa uweze kututambua wanyonge,” ameongeza.

Hapo awali Rais Magufuli alitangaza kutoka Tsh. Milioni 100 kwa ajili ya matibabu ya Mzee Ngoma ambapo aliitaka familia yake kufungua akaunti maalum kwa ajili ya kuingiza fedha hizo haraka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents