Burudani

Undani wa matatizo ya Kanye West yaliyomfanya asitishe ziara yake ya Saint Pablo

Kim Kardashian alikwea ndege kurudi Los Angeles baada ya mume wake Kanye West kulazwa kulinda usalama wake kufuatia matatizo ya uchovu na madhira mengine.

Mandatory Credit: Photo by Andrew H. Walker/WWD/REX/Shutterstock (5585909l) Kanye West Yeezy show, Runway, Fall Winter 2016, New York Fashion Week, America - 11 Feb 2016

Rapper huyo yupo kwenye tathmini ya kisaikolojia katika hospitali ya UCLA Medical Center jijini humo tangu Jumatatu na show zilizokuwa zimesalia za ziara yake yake ya Saint Pablo zimekatishwa huku marafiki zake wakisema amefikia katika hatua ya kutisha, kwa mujibu wa tovuti ya TMZ.

Marafiki pia wameuambia mtandao wa DailyMail.com kuwa mushkeli huo umetokana na matatizo katika ndoa yake na Kim Kardashian, wasiwasi kuhusu kudorora kwa urafiki wake na Jay Z na wivu usiozuilika kwa Beyoncé.

Polisi walipokea wito wa huduma ya kitabibu ulioombwa saa 7 na dakika 20 za usiku kwa saa za Marekani. Alilazwa kutokana na tatizo kubwa la kukosa usingizi na kwamba hiyo ilikuwa muhimu kumweka katika hali salama.Vyanzo vimedai kuwa Kanye alijaribu kukataa kupelekwa kwenye hospitali hiyo na ililazimika afungwe pingu na kuwekwa kwenye kitanda cha wagonjwa(gurney).

Kim alikuwa ametarajiwa kushiriki kwenye hafla katika mji mwingine jioni lakini alilazimika kurejea Los Angeles baada ya taarifa za kushtusha za mumewe kulazwa. Alionekana akishuka kwenye ndege katika uwanja wa Van Nuys Los Angeles, usiku wa Jumatatu na kupanda gari ikiashiria alikuwa akienda UCLA ili kuwa pembeni ya mume wake.

Mashabiki wa Kanye wameanzisha hashtag #PrayForKanye kwenye mtandao wa Twitter tangu kusambaa kwa habari ya kulazwa kwake. Mapema Jumatatu, promota wa ziara ya Kanye, Live Nation, walitangaza kusitishwa kwa show 22 zilizokuwa zimesalia bila kutoa sababu yoyote.

Tangazo hilo limekuja ikiwa ni siku mbili tu baada ya rapper huyo kuondoka jukwaani kwenye show yake baada ya kuzungumza kauli nyingi zenye utata.
West alimponda Hillary Clinton na pia kuwadiss marafiki zake Beyoncé na Jay Z pamoja na Mark Zuckerberg wakati akitumbuiza kwenye show ya Sacramento, Jumamosi.

Marafiki wanadai kuwa tabia hiyo ya Kanye kuzungumza maneno makali dhidi ya watu wengine imemchosha pia mke wake. Wanasema kuwa Kim hakutaka mumewe aendelee na ziara hiyo kwakuwa alitaka awe karibu yake baada ya kuponea chupu chupu kuuawa kwenye tukio la uvamizi huko Paris.

Hata hivyo chanzo kingine kimeiambia DailyMail.com kuwa rabsha hizo za Kanye hazitokani na madawa, bali ni suala la kiakili zaidi. Wanasema wana wasiwasi na hali ya Kim ambaye bado pia hajasahau kabisa tukio la Paris na sasa akihitaji kumliwaza mumewe ambaye kwa kawaida alihitaji zaidi kuliwazwa yeye.

Chanzo kilicho karibu na rapper huyo kimeiambia tovuti ya Page Six kuwa ni mtu anayefanya kazi mno na kwamba kuna wakati huwa halali kwa saa 48 na huweza kuipigia simu timu yake muda wowote usiku.

Wanaamini kuwa maisha ya vurugu ya Kanye pamoja na kifo cha mama yake vimemfanya awe nusu mwendawazimu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents