Michezo

Usain Bolt awaaga mashabiki wake kibabe

Mwanariadha maarufu duniani kutoka Jamaica, Usain Bolt amewaaga rasmi mashabiki wake kushiriki mashindano ya riadha nchini humo kwa kushinda mbio za mita 100.

Tokeo la picha la usain bolt
Usain Bolt

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 30 ambaye ni mshindi wa medali 8 za dhahabu katika michuano ya Olimpiki, ameshinda kirahisi katika mashindano ya mita 100 yaliyofanyika juzi huko Kingstone, Jamaica kwa kutumia sekunde 10.03.

Mbali na ushindi huo aliyoupata juzi, Bolt alikiri kuwa haikuwa kazi rahisi kwa kuwaalijawa na uoga kwa kuogopa kuaga mashabiki wake kwa aibu.

Nimezoea kuona mashindano yote kama kawaida tuu kwani huwa najiamini ila ya leo nimeona migumu sana na nilishikwa na hofu kama ningeshindwa ningeumia sana kuwaaga mashabiki wangu“Alisema Usain Bolt kwenye mahojiano yake na mtandao wa MSN.

Hata hivyo Usain Bolt anatarajia kustaafu mchezo huo mwezi Agosti mwaka huu baada ya mashindano ya dunia ya riadha yatakayofanyika London, Uingereza.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents