Michezo

USAJILI: Chelsea yamng’oa beki wa AS Roma

Mabingwa wa Ligi Kuu ya nichini Uingereza klabu ya Chelsea wameingia kandarasi ya miaka mitano na beki wa timu ya taifa ya Ujerumani, Antonio Rudiger kutoka AS Roma kwa dau la pauni milioni 29.

Mchezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani, Antonio Rudiger 

Rudiger mwenye umri wa miaka 24, alikamilisha uhamisho wake wiki moja baada ya kuisaidia timu yake ya taifa kutwaa ubingwa wa kombe la Mabara.

“Ni jambo linalonifurahisha sana kwa sababu si kila mchezaji anayepata fursa ya kujiunga na klabu kubwa kama hii,” alisema Rudiger.

Ada ya mchezaji huyo inaweza kupanda hadi kufikia pauni milioni 33.3 ukijumuisha na masharti ya mkataba waliyo uingia Chelsea.

“Antonio bado nikijana mwenye umri mdogo lakini anauzoefu katika ngazi ya klabu na kimataifa na ana sifa zote ambazo zinahitajika kucheza likgi ya Uingereza.

Rudiger alichezea timu ya vijana Borussia Dortmund kabla ya kuhamia Stuttgart mwaka 2011.

Kwa mara ya kwanza alicheza ligi ya Bundesliga ya nchini Ujerumani mwezi Januari mwaka 2012 kabla ya kuhamia Roma 2015.

Rudiger alicheza mechi 30 za Serie A msimu wa 2015/6 akiwa na klabu ya Roma na kuwasaidia kumaliza nafasi ya tatu na kisha mechi 26 msimu wa 2016-17 walipomaliza nafasi ya pili katika mimano wa ligi baada ya Juventus.

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents