Habari

Utafiti: Kulala zaidi ya saa 1 mchana kunaongeza hatari ya kuugua kisukari

Kupata walau saa moja ya kuuchapa usingizi mchana, ni tamanio la wafanyakazi wengi walio busy.

woman-asleep-at-computer

Lakini timu ya wanasayansi imeonya kuwa kujiruhusu kupata lepe refu la usingizi mchana kunaweza kukuongezea hatari ya kupata ugonjwa wa Kisukari. Wamesema wale wanaolala kwa zaidi ya saa moja kwa siku, wana asilimia 45 ya kupata ugonjwa huo mbaya, watafiti wamebaini.

Hata hivyo kulala kwa muda mfupi, hakukuonesha hatari zozote, kwa mujibu wa utafiti huo uliowasilishwa kwenye mkutano wa Umoja wa Ulaya kwa tafiti za kisukari, (EASD) huko Munich, Ujerumani.

Wataalam kutoka Japan, waliangalia taarifa kutoka tafiti 21 zilizohusisha watu 300,000 na kukuta uhusiano kati ya ulalaji wa mchana na kisukari. Waligundua kuwa kulala kwa zaidi ya saa nzima kunawaweka watu katika hatari ya kuupata ugonjwa huo.

Lakini wale wanaolala chini ya saa moja, hawakuwa kwenye hatari hiyo.

Walielekeza pia kuwa kulala vizuri ni sehemu muhimu ya maisha yenye afya pamoja na chakula bora na mazoezi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents