Burudani

Utafiti: Sikiliza ‘In Da Club’ ya 50 Cent kabla ya kuingia kwenye usaili wa kazi , utafanya vizuri

Utafiti uliofanywa na ‘Society For Personality And Social Psychology’ umedai kuwa kusikiliza nyimbo zenye mdundo au base kubwa huwasaidia wanaosikiliza kujiamini zaidi wakati wa usaili wa kazi au mkutano.

50cent_070313

Watafiti hao walicheza nyimbo kwa makundi ya watu maalum na kupata mrejesho. Waligawa nyimbo katika makundi mawili “high-power” na “low-power” ambapo mfano wa nyimbo za “high-power” ni pamoja na wa 50 Cent “In Da Club,” wimbo wa Queen “We Will Rock You,” na wa 2 Unlimited, “Get Ready For This” wakati mfano wa nyimbo za “low-power” ni pamoja na wimbo wa Biggie, “Big Poppa,” Fatboy Slim’ “Because We Can,” na ule Baha Men’s “Who Let The Dogs Out?”

Watafiti hao walidai kuwa watu wa kundi la kwanza lililosikiliza wimbo 50 Cent, In Da Club, na zingine za kundi la high-power, walionekana kuwa na udhibiti wa mazingira kama usaili wa kazi au mkutano na wateja.

Walibainisha kuwa nyimbo za “Low power” kama ule wa Notorious B.I.G.’s “Big Poppa,” humfanya mtu kuwa muoga na asiyechangamka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents