Habari

Uturuki yamuonya vikali mbabe wa kivita wa Libya Jeneral Khalifa Haftar

Uturuki imesema kuwa vikosi vya kiongozi wa Libya Khalifa Haftar ”vitalengwa” ikiwa hawatawaacha huru haraka raia sita wa Uturuki. Vikosi vya Jenerali Haftar vilisema siku ya Ijumaa kuwa vitashambulia maslahi ya Uturuki kwa kuwa taifa hilo linaunga mkono serikali ya Libya inayoungwa mkono na jumuia ya kimataifa.

Moshi ukitoka kwenye majengo kutokana na mashambulizi ya anga

Pia walidai kuwa waliharibu ndege isiyo na rubani ya Uturuki kwenye anga la Tripoli.

Libya imekumbwa na machafuko na mgawanyiko tangu kuondolewa madarakani na kuuawa kwa aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo, Muammar Gaddafi mwaka 2011.

Jenerali Haftar alianza mashambulizi dhidi ya serikali inayotambuliwa na jumuia ya kimataifa,(GNA) inayoongozwa na waziri mkuu Fayez al-Sarraj, mwezi Aprili.

Wapiganaji wanaounga mkono serikali inayotambuliwa kimataifa wakifyatua risasi

Kwanini Haftar na Uturuki ziko kwenye mzozo?

Uturuki inaunga mkono GNA, inapeleka ndege zisizo na rubani, silaha na magari kwa ajili ya kusaidia juhudi za serikali kupambana na vikosi vya Jenerali Haftar, ambavyo vinadhibiti sehemu kubwa ya mashariki na kusini mwa Libya.

Jenerali Haftar kutoka jeshi la taifa la Libya (LNA) amesema atashambulia meli za Uturuki kwenye maji ya Libya na maeneo muhimu ya kibiashara ya Uturuki.

Pia amezuia ndege za kibiashara kutoka Libya kwenda Uturuki.

Mapema siku ya Jumapili, Uturuki ilisema ”italipa kisasi kwa kuchukua hatua kali zaidi” kwa vitisho vyovyote kutoka kwa vikosi vya Jenerali Haftar.

Waziri wa ulinzi wa Uturuki, Huluski Akar ameonya kuwa vikosi vya LNA vya Libya vitalipa mashambulizi yoyote watakayofanya dhidi ya maslahi ya Uturuki.

Uturuki imesema inataka kupunguza mapigano dhidi ya Jenerali Haftar, ambaye anaungwa mkono na Umoja wa falme za kiarabu na Misri.

Siku ya Alhamisi, GNA ilichukua mji muhimu wa Gharyan, mji ambao ni ngome ya vikosi vya bwana Haftar.

Kwanini kuna mapigano Libya?Rais wa zamani wa Libya Muamar GaddafiHaki miliki ya pichaREUTERS

Kanali Gaddafi aliongoza Libya kwa miongo minne mpaka jeshi lilipomuondoa madarakani mwaka 2011.

Tangu wakati huo, hakuna mamlaka iliyokuwa na udhibiti kamili wa nchi hiyo.

Makundi kadhaa ya kisiasa na kijeshi wanavutana lakini hasa ni Bwana Sarraj na Jenerali Haftar.

Jenerali Haftar ni nani?

Khalifa Haftar jina lake limekuwepo sana kwenye siasa za Libya kwa zaidi ya miongo minne na alikuwa mshirika wa karibu wa Gadaffi mpaka ulipotokea mgogoro mwaka 1980, ambao ulimlazimu kwenda kuishi uhamishoni nchini Marekani.

Jenerali huyo alirejea Libya wakati wa maandamano mwaka 2011 na kuwa kamanda muhimu wa kikosi cha mapinduzi Mashariki mwa LibyaJenerali Khalifa Haftar

Raia wa Libya wana hisia mchanganyiko kumhusu yeye kutokana na uhusiano wake na Gadaffi na Marekani.

Vikosi vya Jenerali Haftar vinaungwa mkono na Ufaransa, Misri na Umoja wa falme za kiarabu. Mwezi Aprili, Rais wa Marekani Donald Trump,alionekana kumuunga mkono lakini shauku yake imepoa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents