Habari

TANZIA: Afisa Mtendaji Mkuu wa Safaricom,Bob Collymore aaga dunia

Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni kubwa zaidi ya mawasialiano ya simu Afrika Mashariki Safaricom, Bob Collymore ameaga dunia, kampuni hiyo imethibitisha.

Afisa Mtendaji wa Safaricom Bob Collymore

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Safaricom, Collymore amefikwa na umauli asubuhi ya leo Jumatatu Juni Mosi 2019 nyumbani kwake jijini Nairobi.

Mwenyekiti wa kampuni hiyo Nicholas Ng’ang’a amesema kuwa afya ya Collymore ilikuwa mbaya majuma ya hivi karibuni.

Collymore, alichukua likizo ya matibabu ya miezi tisa mwishoni mwa mwaka 2017 na kuelekea nchini Uingereza kwa ajili ya matibabu ya saratani .Alirejea Kenya mwezi Juni mwaka jana. Gazeti la Standard media nchini Kenya limeripoti.

Marehemu ameacha mke na watoto wanne.

Collymore alianza kuongoza gurudumu la Safaricom mwaka 2010 kutoka kwa Michael Joseph ambaye kwa sasa ni mmoja wa wajumbe wa bodi ya kampuni hiyo, pia mwenyekiti wa bodi ya shirika la ndege la Kenya Airways.

Mwaka 2017 wanahisa walipiga kura kuongeza mkataba wa Bob Collymore kwa miaka miwili baada ya mkataba wake kuisha. Mkataba aliokuwa akiufanyia kazi ulikuwa unatarajiwa kufikia tamati mwaka 2020 na kumfanya kuwa Mkurugenzi aliyekalia kiti hicho kwa muda mrefu zaidi kwenye historia ya kampuni hiyo.

Viongozi kadhaa wakiwemo Rais Uhuru Kenyatta wametuma salamu za rambirambi kwa familia kutokana na kifo hicho.

Uhuru amesema nchi imepoteza kiongozi ambaye mchango wake kwa Kenya utakumbukwa.

”Ni huzuni kuwa asubuhi hii nimepokea taarifa za kifo cha Mkurugenzi wa Safaricom bwana Bob Collymore baada ya miaka kadhaa ya kupambana na saratani.Nchi imepoteza kiongozi ambaye mchango wake kwa Kenya utakumbukwa,” alisema Rais Uhuru Kenyatta.

Rais Uhuru Kenyatta atuma Salamu za rambirambi

”Ni huzuni kuwa asubuhi hii nimepokea taarifa za kifo cha Mkurugenzi wa Safaricom bwana Bob Collymore baada ya miaka kadhaa ya kupambana na saratani.Nchi imepoteza kiongozi ambaye mchango wake kwa Kenya utakumbukwa,” alisema Rais Uhuru Kenyatta.

Rais Kenyatta amesema Bob Collymore alikuwa kiongozi ambaye aliiongoza Safaricom katika nafasi kubwa ya kuwa kampuni yenye matunda makubwa zaidi Afrika Mashariki.

Ametoa salamu za pole kwa familia ya marehemu,marafiki na wafanyakazi wa Safaricom,

Mbali na kutumikia nafasi yake akiwa Safaricom, amesema Collymore alitoa ujuzi wake wa kiutawala katika kutekeleza ajenda ya maendeleo ya taifa.

Chanzo Shirika la habari la BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents