Michezo

Tetesi za soka barani Ulaya, Pep Guardiola atilia wasi wasi uwezo wa Neymar, Lukaku kumpisha Ben Yedder Man United, Madrid kumtoa Asensio kwaajili ya Mane

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema hana uhakika kama Neymar, 27, atakuwa na makali yaleyale aliyokuwa nayo kabla atakaporejea klabu ya Barcelona  Paris St-Germain. (Ara, via Mirror)

Neymar

Manchester United wameshaafikiana kuhusu matakwa binafsi na mshambuliaji wa Sevilla Wissam Ben Yedder, 28. Mshambuliaji huyo raia wa Ufaransa anatarajiwa kujiunga na mashetani hao Wekundu endapo mshambuliaji wa Ubelgiji Romelo Lukaku atauzwa ama la. (Express)

Manchester United wanaweza kuwapoka Tottenham tonge mdomoni katika usajili wa kiungo wa klabu ya Lyon ya Ufaransa, Tanguy Ndombele. Spurs tayari wameshakubali kumnunua mchezaji huyo lakini hawajamalizana naye kuhusu matakwa yake binafsi mchezaji huyo mwenye miaka 22. (L’Equipe, via Metro)

Coutinho

Liverpool wanaweza kumrudisha kiungo mshambuliaji wa Brazil Philippe Coutinho, 27, baada ya mchezaji huyo kushindwwa kuwa na wakati mzuri kwenye klabu ya . (Le10 Sport, via Mirror)

Kiungo wa Aston Villa John McGinn anaweza akatakiwa na Manchester United, ambao itawabidi walipe kitita cha pauni milioni 50 kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uskochi. (Sun)Sadio Mane

Real Madrid wanataka kuwapa Liverpool kiungo Mhispania Marco Asensio, 23, lakini wanataka mshambuliaji machachari wa Senegal Sadio Mane, 27, awe sehemu ya mabadilishano hayo. (Express)

Tottenham wanatarajiwa kumpeleka kwa mkopo kiungo wake kinda Jack Clarke 18, katika klabu yake ya zamani ya Leeds United. (Guardian)

Derby County wanapanga kumsajili mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi Phillip Cocu kama kocha atakayerithi mikoba ya Frank Lampard ambaye anatarajiwa kujiunga na klabu ya Chelsea muda wowote ule. (Times – subscription required)Frank Lampard

Leeds wanataka kumsajili mshambuliaji wa Ecuador Felipe Caicedo, ambaye anachezea klabu ya Lazio ya Italia na ameshawahi kuchezea klabu ya Manchester City. (Imperio, via Star)

Klabu ya Juventus inapanga kumsajili winga wa kinda wa Burnley na England, Dwight McNeil, 19. (Sun)

Juventus pia inataraji kuwauza viungo wake wawili Blaise Matuidi na Sami Khedira wote wenye miaka 32. (Tuttosport, via Calciomercato)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents