Habari

UVCCM waiomba Takururu kuwakaba watoa rushwa

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), umeiomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kufuatilia mwenendo wa wagombea wake wa uchaguzi ngazi ya taifa ili kuhakikisha uchaguzi huo unapata viongozi kwa njia halali na sio kwa kutoa rushwa.

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka.

Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaam na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya uchaguzi wa umoja huo.

Kuna wagombea ambao wanadhani watashinda kwa rushwa. Sisi tunasema mgombea au mpigakura yeyote atakayethibitika kutoa au kupokea rushwa hatua za kimaadili na kisheria tunaelekeza zichukuliwe ili kulinda heshima ya taasisi yetu,” amesema Shaka.

Hata hivyo, umoja huo umesema hadi sasa wamejitokeza wanachama wao 113 kuwania nafasi ya Mwenyekiti inayoshikiliwa na Sadifa Hamis Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents