BurudaniVideos

Vanessa Mdee aonjesha ladha tofauti ya album yake Money Mondays (Video)

Mara ya mwisho nimeongea na Vanessa Mdee nilimtania kuwa album yake ‘Money Mondays’ inaanza kuwa kama ‘Detox’ ya Dr Dre iliyosubiriwa kwa takriban miaka 10 na baadaye akashindwa kuitoa.

13714123_623292121172485_1736413441_n

Hata hivyo Vanessa alidai kuwa album hiyo aliyoanza kuisema kwa takriban miaka miwili sasa, itatoka na yupo kwenye maandalizi makali kuhakikisha mashabiki wanapata kitu bora.

Jumatano hii ameshare video kwenye Instagram ikimuonesha akiwa studio na unasikika wimbo wa taratibu ambao unanifanya niweza kuwa huenda Vee anatuonesha upande wa pili wa aina ya nyimbo zitakazokuwemo kwenye album hiyo.

Akiweka emoji ya love, Vanessa aliandika tu, “#MoneyMondays.” Tazama video hiyo chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents