Burudani

Video: Belle 9 adai waongozaji wa Bongo na location nzuri za nyumbani zinamshawishi kutofikiria kwenda kufanya video nje

Belle 9 anadhani Tanzania ina waongozaji wakali na location za kuvutia kufanya video za muziki kiasi ambacho haoni sababu ya kusafiri kwenda kufanya video zake nje ya nchi.

Muimbaji huyo aliyeachia video ya wimbo wake ‘Shauri Zao’ hivi karibuni, amesema uwezo wa waongozaji wa Tanzania akiwemo Hanscana unatosha kabisa kumpa video yenye ubora.

https://www.youtube.com/watch?v=BiwaZPqlPVk

Amesema kama wasanii wa Tanzania watafanya video nzuri kutumia waongozaji na location za nyumbani, zitawavuta pia wasanii wa nje kuja kufanya video zao nyumbani.

“Cha msingi zaidi naona ni userious tu, tunaweza kukaa na kukutana na waongozaji ambao kweli wana hiyo nia na hasira ya kufanya zaidi ya vile wanafanya,” amesema Belle.

“Kwasababu kama mtu yuko tayari kupokea changamoto na pia kama anahitaji kupiga hatua ni vizuri sana kujitoa katika kile kitu anachofanya. Kama director Hanscana amejitoa kwa asilimia zile na tayari imereflect vizuri ni muda sasa wa kubalisha huu mfumo wa watu kama wanaweza kwenda South Africa basi watu watoke huko waje huku, watu watoke Ghana waje huku, watu watoke Nigeria waje huku,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents