Burudani

Video: Hakuna siri tena kati ya Drake na Rihanna

Drake na Rihanna hakuna siri tena – wameonyesha mapenzi moto moto.

Rihanna

Ni muda mrefu wawili hao wamekuwa wakihusishwa kuwa na mahusiano lakini hakuna aliyethibitisha mpaka sasa kati yao kama ni wapenzi. Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umedai kuwa wawili hao wameonekana mjini Miami Jumanne hii kwenye klabu ya usiku ya E11EVEN wakila bata pamoja.

Siku chache zilizopita Drake alianza kuonyesha dalili za mahusiano yake na mrembo huyo baada ya kununua bango kubwa la barabarani na kuandika ujumbe wa kumpongeza Rihanna. Lakini stori kubwa zaidi ilikuwa wikiendi iliyopita kwenye tuzo za MTV VMA, Drake alikiri kuwa amekuwa akimpenda Rihanna tangu akiwa na miaka 22.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents