Michezo

Video: Leon aibukia Manyara kabla ya mchezo na Gor Mahia

Kueleka mchezo wa kirafiki baina ya Everton FC dhidi ya mabingwa wa SportPesa Super Cup, Gor Mahia, Nguli na balozi wa klabu hiyo ya nchini Uingereza, Leon Osman ameendelea kutembelea vivutio mbalimbali hapa nchini kabla ya mchezo wao wa Julai 13 utakao chezwa katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam.

https://www.instagram.com/p/BWZrShaHHVv/?taken-by=tzsportpesa

Leon alipata nafasi ya kutembea juu ya daraja linaloshikiliwa na kamba ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Manyara.

Osman ambaye aliwasili wikiendi iliyopita kutoka nchini Uingireza alipata nafasi pia ya kumbelea makaburi ya Jumuiya ya Madola yaliyopo eneo la makumbusho kwa kuweka mashada ya maua.

Tayari homa ya mpambano huo miongoni mwa mashabiki nchini imeendelea kuwa kubwa zaidi huku wengi wakiwa na shauku ya kuwaona nyota mbalimbali wa Everton kama vile Wayne Rooney, Jordan Pickford, Ross Barkley, Idrissa Gana Gueye na wengine wengi.

Viingilio vya mchezo huo ni Sh 8000/= kwa VIP C na Sh 3000/= kwa viti vya mzunguko na mchezo unatarajiwa kuanza majira ya saa 11 jioni.

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents