Habari

Video: Maisha ya kifahari ya mfanyabiashara Alex Massawe anayetafutwa na Interpol

Dola za Kimarekani, magari ya kifahari, mijengo yenye hadhi ya mahekalu ndio maisha ya mfanyabiashara maarufu kutoka Tanzania, Alex Massawe anayetafutwa na polisi wa kimataifa, Interpol.

Video iliyowekwa kwenye mtandao wa Instagram inamuonesha mfanyabiashara huyo akiendesha gari la kifahari lenye thamani ya dola 120,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 200.

“Hello guys you can see here is Mr Alex Massawe is driving a 120,000 US dollar car, we like to drive a good shit,” anasema mpambe wake aliyekaa kwenye kiti cha abiria ndani gari hilo huku Massawe akionekana akitoa lundo kubwa la noti za dola 100 za Kimarekani kumpa.

“As you can see this is shopping money that he can shop for just shoes and clothes for the day it’s Sunday so we do some Nike shopping, some gold shopping. But this money is not a lot for him,” anaongeza mpambe huyo.

Taarifa zinadai kuwa mfanyabiashara huyo anaishi nchini Afrika Kusini. September mwaka jana magazeti ya Tanzania yaliandika taarifa za kukamatwa kwake na kwamba angeletwa nchini kupandishwa kizimbani kwa makosa yanayomkabili yakiwemo ya mauaji. Hata hivyo Interpol Tanzania ilikanusha taarifa za kukamatwa kwake.

Massawe alitoroka nchini baada ya kuhusika kwenye mauaji akishirikiana na mfanyabiashara mwenzake, Abubakar Marijani maarufu kama Papaa Msofe ambaye yupo jela.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents