Burudani

Agnes Masogange apata uraia wa Afrika kusini na kubadili jina, sasa aitwa ‘Thando’

Video vixen maarufu wa Bongo Agnes Gerald maarufu zaidi kwa jina la Agnes Masogange ambaye kwa miezi kadhaa sasa amehamishia makazi yake Afrika Kusini, amebadili jina na huenda akawa raia wa huko!

Aggy3

Kupita Instagram mrembo huyo mwenye umbo ‘matata’ alianza kwa kupost picha ya pasi ya kusafiria ya Afrika Kusini kama ishara kwamba amepata uraia mpya wa nchi hiyo.

Agnes msauzi

Kuthibitisha kile ambacho kila mmoja alifikiria (kuwa amebadili uraia) Masogange baada ya muda mfupi aliandika kuhusu kubadili na jina pia. “My new name is thando not Agnes any more”

Aggy4

Hivi karibuni Bongo5 ilikutana uso kwa uso na Agnes Thando jijini Durban, Afrika Kusini kwenye tuzo za MTV MAMA 2014, na katika mahojiano alisema kuwa kwa sasa amehamia kabisa Afrika Kusini na makazi yake yako jijini Johannesburg.

Kutokana na sheria za Tanzania ambazo haziruhusu uraia wa nchi mbili, hii inamaanisha Thando si mbongo tena?

Sogeza hadi dakika ya 0:24 alipozungumzia kuhamia kwa Madiba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents