Burudani

Video: Mfahamu Rin Marii wa ‘Salaam’ anayetabiriwa makubwa

Doreen Maryanne Paul aka Rin Marii ni msanii wa kike anayetazamwa kuweza kufika mbali zaidi kupitia muziki wake kutokana na uwezo wake alioanza kuuonyesha kupitia wimbo wake mpya ‘Salaam’.

Msanii huyo akiongea na Bongo5 amesema, ameanza kufanya muziki mwaka 2014 baada ya kuhakikisha amefikia malengo yake ya kupata elimu aliyokuwa anainata hapo mwanzoni. Lakini pia amedai ilikuwa ni ngumu kuishawishi familia yake iweze kumruhusu aingie kwenye tasnia ya muziki.

Muimbaji huyo amefunguka kuwa wimbo wa ‘Salaam’ umeandikwa na Goodluck Gozbert maarufu kama Lollipop ambao tayari ulikuwepo studio lakini hata hivyo amedai kuna nyimbo ambazo zipo tayari ameshaziandika mwenyewe hajaziachia.

“’Salaam’ ni ngoma ambayo sijaandika mimi, nilienda pale Africa Studio nikaikuta nikaipenda nikaona niifanye kama ngoma yangu ya kwanza. Niliipenda kwa sababu ina ujumbe wa kujishusha na kuomba msamaha. Ni kitu ambacho niliona ni kitu cha utofauti na hakijaimbwa hapa nyumbani. Nina nyimbo kadhaa nimeziandika mwenyewe na hizo zitatoka mbeleni Mungu akipenda,” amesema muimbaji huyo.

Akiwataja wasanii ambao wamemvutia kuingia katika muziki, msanii huyo amesema, “Nianze na wasanii ambao nilikuwa nawasikiliza wakati mimi nakuwa kama Jay Dee, Kulikuwa na Unique Sisters kipindi kile, kina mwana FA na AY. Miaka ilivyokuwa inazidi kusogea na vile kulivyokuwa na wasanii wapya na mimi ndio nikazidi kupenda kama vile kina Diamond, Vanessa Mdee, Maua Sama, Nandy, Ruby, kila mtu anakuwa na kitu chake cha pekee ambacho kinanivutia kinanifanya na mimi niingie katika hii industry.”

Marii amewataja wasanii ambao anatamani kufanya nao kazi ni pamoja na Diamond, Weusi, Ruby, Nandy, Jay Dee na Upendo Nkole.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents