Burudani

Video: Seline awatolea uvivu walokole wanaombeza

Msanii wa muziki ambaye awali alikuwa akifanya muziki katika kundi la The Industry, Seline amefunguka juu ya changamoto na kashkash anazokutana nazo toka atangaze kuhamia katika maisha ya kilokole.

Akiongea na Bongo5, Seline amesema kuwa maisha yake ya wokovu hayajamfanyaabadirike kama watu wanavyodahni na pia wokovu ni jambo lililopo ndani ya moyo wa mtu.

“Nilivyokuwa nafikiria neno kuokoka na nilivyoingia maisha ya wokovu it’s a big difference, cha kwanza nilisema kuwa nafanya muziki wa Injili na inspertation songs, which means nataka kuhamasisha jamii na kumtumikia mungu. Kitu ambacho watu wanakosea ni kuwa mlokole is bean born again ndani ni moyo, nilichogundua watu wengi wanafanya kumpress jamii, watu wengi tumeokoka tunafanya gospel mtu anahofu kuwa jamii inanichukuliaje nikifanya hivi na hivi jamii itakataa , nikifanya hivi jamii inaniangaliaje kama msanii wa injili,” amesema msanii huyo.

Pia akaongeza kuwa ulokole wake ni aliamua kumfanyia mungu na ndiyo anajua  nini kipo ndani yake moyo wake, hata kama hakuna anayeona na kuamini.Vile vile amsisitiza kuwa licha ya jamii kumbeza ila atabaki kuiheshimu kama kawaida kwa sababu wanamzunguka ila anafanya hivyo kwa sababu ya kumtumikia mungu.

Na Salum Kaorata

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents