Video ya Alikiba na Rudy boy wa P Square kutoka kesho, wame-shot video Lagos Nigeria (+ Video)

Siku ya kesho Jumatano ndio siku rasmi ambayo video ya ngoma ya Alikiba #Salute itaachiwa rasmi ambapo katika ngoma hiyo amemshirikisha msanii kutoka nchini Nigeria Rudy boy ambaye alikuwa mmoja wa waliokuwa wanaunda kundi la P Square.

Ngoma hiyo imeweka attention kubwa sana mtandaoni kutokana na aina ya wasanii waliopo kwenye ngoma hiyo pia muonekano wa mavazi waliyovaa yakiendana na jina la wimbo ambalo ni #Salute yakiwa ya kijeshi.

Kwa taarifa za kutoka katika menejimenti ya Alikiba ni kwamba video ya ngoma hiyo ya #Salute imerekodiwa katika jiji la Lagos nchini Nigeria kipindi ambacho Alikiba alienda Lagos hivyo waliamua kufanya kila kitu kutokana na ratiba za wasanii wote wawili ili kuepusha usumbufu. kila kitu kimefanyikia Lagos Nigeria.

Mashabiki wengi wa Alikiba wamekuwa wakisubiria kwa hamu video ya ngoma hiiya Salute kuiona ilivyo na hiyo yte ni kutokana na ukubwa wa wasanii wote wawili Alikiba pamoja na Rudy boy lakini pia ujio wa Alikiba umekuwa wa kitofauti sana kwani ndani ya wiki moja aliachia ngoma mbili moja ikiwa ni NDOMBOLO ambayo ameshirikiana na wasanii wote wa Kings Music na hii ya #Salute bila kusahau wiki mbili nyuma kabla ya kuiachia Ndombolo alishirikishwa na Barnaba kwenye ngoma ya Cheketua.

Kupitia Instagram ya Alikiba ameandika kuwa Kesho ndio video ya #Salute inatoka rasmi ambapo aliandika kwamba: “You Asking for the Video!? Me and my brother General @iamkingrudy shot a Movie of the Year for our song SALUTE !! And its Officially Dropping on Wednesday 30th of June .Enjoy the Trailer 🎥🔥
#Salute
#KingKibaXKingRudy
#KingKiba

https://www.instagram.com/p/CQskc_ZBjVI/

Related Articles

Back to top button