BurudaniVideos

Video ya Diamond ya wimbo ‘Mtasubiri’ akiwa na Zuchu yapigwa ‘stop’ na TCRA

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeagiza kusitishwa kwa video ya wimbo wa Diamond Platnumz ft. Zuchu “mtasubiri” kutokana na kipande kinachoonesha Zuchu akiwa Kanisani kwenye kwaya kisha kuacha kuimba na kupokea simu.

Taarifa iliyotolewa na TCRA imesema “kipande hicho cha video kimeleta ukakasi miongoni mwa Waumini wa madhehebu ya dini na kuleta hisia kwamba ni dharau juu ya dini/madhehebu fulani hivyo kwa barua hii TCRA inaagiza vyombo vyote vya utangazaji na mitandao ya kijamii hapa nchini kutorusha video ya wimbo huo hadi hapo Msanii tajwa (Diamond Platnumz) atakaporekebisha sehemu hiyo ya video”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents