Fahamu

Vifahamu vyuma vitano vya ajabu vilivyotokea duniani hivi karibuni

Chuma cha kwanza cha ajabu kugundulika duniani katika miaka ya karibuni ni kile cha Utah kilichoonekana mwezi Novemba 18, 2020.

Chuma hicho kilionekana katika maeneo ya jangwa nchini Marekani na kisha kikapotea chenyewe, maafisa walieleza.

Ripoti za kuaminika zilieleza kuwa kiliondolewa na watu ambao hawakujulikana.

Urefu na muonekano wa chuma hicho ni sawa kabisa na hiki kilichoonekana wiki iliyopita nchini DRC, chuma hicho kina futi 12(3.7m).

Chuma hicho kilivutia wageni wengi kwenda kukiangalia na kupiga picha.

Hakuna mtu aliyesema kuwa amekipandikiza chuma hicho mpaka kilivyopotea.

Mamlaka katika jimbo la Utah nchini Marekani ziliachwa mdomo wazi baada ya kupatikana kwa kifaa cha chuma kisichokuwa cha kawanda katika eneo la jangwani.

Chuma hicho cha kushangaza kilipatikana na kundi la maafisa wakutoa huduma ya kulinda wanyamapori waliokuwa wakisafiri kwa kutumia ndege aina ya helikopta.

Walikuwa wakitumia ndege hiyo kuhesabu kondoo katika eneo la mashambani kusini mashariki mwa Utah, ndipo walipoona kifaa ambacho sio cha “kawaida”.

Wanasema kifaa hicho kilikuwa kimechimbiwa chini kati ya miamba mikukbwa.

Haijabainika ni nani alikiweka hapo kifaa hicho cha chuma, kilicho na urefu wa karibu mita 3.6.

“Ni kitu ambacho sikuwahi kukiona tangu nilipoanza kufanya kazi hii,” alisema rubani wa helikopta hiyo Bret Hutchings katika mahojiano na televisheni ya eneo hilo KSLTV.

Hutchings alisema wanabiolojia waliokuwa wakihesabu kondoo wakiwa kwenye helikopta kwanza waliona kifaa hicho wakiwa angani.

“ANa kusema, ‘Subiri, subiri kidogo, hebu geuka urudi tulikotoka,!’ Nakauliza, ‘Kuna nini?’ Akasema, ‘Nimeona kitu huko nyuma, naomba turudi tukaangalie! ‘”Alirudia kusema rubani huyo.

Funcionarios de vida silvestre alejándose del monolito.

Mamlaka ya usalama wa umma huko Utah, katoa picha ya kifaa hicho katika taarifa kwa vyombo vya habari wiki iliyopita.

Taarifa hiyo ilisema mamlaka zinatathmini ikiwa “kutakuwa na haja ya kufanya uchunguzi zaidi.”

“Ni hatia kuweka kifaa ambacho hakijaidhinishwa au mchoro katika ardhi ya umma iliyotolewa na serikali, haijalishi ni katika sayari ipi,”ilisema taarifa hiyo.

Mamlaka hata hivyo haijafichua ni wapi hasa kifaa hicho kilipatikana, kwa kuhofia watafiti huenda wakakitafuta na pengine “wakwame nacho.”

Kufikia sasa hakuna aliyejitokeza kusema kama alihusika kuweka kifaa hicho katika sehemu hiyo.

Ili kutafuta majibu ya maswali yaliyoibuka, baadhi ya watu wa jimbo la Utah waliingia katika mitandao ya kijamii, na kuweka jumbe katika mtandao wa Instagram: “Twaomba kujua hii ni nini? Kuna yeyote anayejua?”

Kitu cha kushangaza ni kwamba kuna kitu kinachofanana na sanamu za msanii marehemu John McCracken ambacho kimegunduliwa katika eneo hilo hilo la jangwani la Utah.

Lakini baadhi ya watu waliangazia nadharia za kushangaza kuelezea kifaa hicho kilifika vipi mahali hapo.

“Naomba tuachane na kifaa hicho tuendelee mbele na maisha yetu. Na sio kumfuafuta shetani wakati mbaya zaidi wa maisha yetu,” aliandika mwingine.

White spacer

Baadhi ya watu waliweka picha katika mitandao ya kijamii kuonesha chuma hicho cha ajabu kisichojulikana asili yake.

Chuma cha Glastonbury Tor

c

Desemba 9, 2020, chuma kingine cha ajabu chenye muonekano unaofanana ya chuma cha Utah kilionekana juu ya Glastonbury Tor.

Watu waliokishuhudia wanasema waliona chuma hicho kikubwa kimejilaza juu ya mlima, inawezekana kiliwekwa majira ya usiku.

Michelle Cowbourne ambaye alishuhudia anasema “Sikuamini macho yangu kuwa nimeona kitu kama hicho” wakati alipokiona kwenye eneo la hifadhi ya taifa.

Tangu chuma cha ajabu kionekane na kupigwa picha mwezi Novemba, huko Utah vyuma vya aina hiyo hiyo vimekuwa vikijitokeza katika maeneo mbalimbali duniani.

b

Chuma kilichoonekana katika maeneo ya fukwe za Isle of Wight kiliondolewa na kuuzwa

b

Mwezi huo huo wa Desemba mwaka jana chuma kingine kinachofanana na kile kilichoonekana Marekani na Romania, kiligundulika katika fukwe za Isle of Wight nchini Uinngereza.

Baada ya kugundulika kiliondolewa na kuuzwa.

m

Chuma cha ajabu kilichotokea Dartmoor Uingereza

CHUMA

Desemba 10, Chuma kingine cha ajabu kilionekana katika milima ya Dartmoor nchini Uingereza.

Chuma hicho kilichokuwa na muonekano wa ajabu kiligundulika katika eneo la mbuga ya taifa karibu ya kijiji cha Throwleigh.

Mark Bullock, ambaye alikishuhudia chuma hicho anasema kilionekana kama kuna mlimani na kuonesha kama kuna tatizo kwenye anga.

Chuma hiki ni cha tatu kuonekana nchini Uingereza ndani ya siku kadhaa, kuna kingine kilitokea Isle of Wight na kingine Glastonbury.

Bwana Bullock, ambaye huwa anatembea milima ya Dartmoor kila mara anasema chuma hicho chenye muundo wa pembe tatu hakikuepo na kinaonesha tofauti na vyuma vingine kwasababu hiki kinaonesha kama kuna shida katika anga.

CHUMA

Hata hivyo bwana Bullock ameelezea kuwa ukikaribia chuma hicho ni kama kimetengenezwa na binadamu.

“Ukikikaribia kwa karibu unaweza kugundua kuwa kimetengenezwa tu na wala hakijatokea dunia nyingine kama inavyodhaniwa.”

Mbuga ya taifa ya Dartmoor ilithibitisha kuondoa chuma hicho ili kuondoa hatari yoyote inayoweza kusababisha athari katika mazingira ya mbuga.

Chuma cha ajabu kimeonekana DRC

Watu wakikishangaa chuma cha ajabu kilichoonekana mjini Kinshasa

Chuma cha ajabu kilichoonekana katika eneo la makutano ya barabara jijini Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kimeteketezwa na moto kwa kuhofia uasili wa chuma hicho.

Watu mjini Kinshasa, wamekipiga mawe na kukichoma chuma hicho cha ajabu cha kung’aa chenye futi 12 ambacho kinafanana na vyuma kadhaa ambavyo vimekuwa vikionekana duniani kote miezi ya hivi karibuni, cha kwanza kilionekana Utah nchini Marekani mwezi Novemba mwaka jana.

Wengi walipokiona walianza kwa kukipiga picha na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Hata hivyo, wengi walihofia imani za nguvu za giza.

“Tumeamka tu na kuona chuma hiki cha ajabu cha pembe nne… Tulishangazwa kwasababu ni chuma ambacho huwa tunakiona kwenye makala kuhusu freemasons au illuminati,” mkazi mmoja wa eneo hilo Serge Ifulu aliiambia Reuters.

Uvumi kuhusu chuma hicho ambacho ulianza kusambaa katika mji wa Bandal mwishoni mwa wiki iliyopita lakini Jumatano wakaanza kukiteketeza.

drc
Watu wakikiteketeza chuma cha ajabu kilichoonekana mjini Kinshasa

Kundi la watu waliokusanyika Jumatano walikiteketeza chuma hicho huko DRC.

Walioshuhudia tukio hilo wanasema watu walitaka kujua kuna nini ndani ya chuma hicho baada ya kukichoma walikuta kuna vyuma tu.

Meya wa eneo hilo Bayllon Gaibene ameliambia shirika la BBC kuwa wametuma sehemu ya chuma hicho kwa wanasayansi ili kijulikane kilipotokea.

Na alikanusha madai yanayomshutumu Gavana wa Kinshasa Gentiny Ngobila kuhusika na kutokea kwa chuma hicho cha ajabu.

Credit by BBC.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents