Burudani

Virusi vya Corona vyazidi kuenea kwa kasi, Yapelekea show za wasanii Mariah Carey Stormy, kundi la korea BTS na wengine kufutwa – Video

Virusi vya Corona vyazidi kuenea kwa kasi, Yapelekea show za wasanii Mariah Carey Stormy, kundi la korea BTS na wengine kufutwa - Video

Staa wa muziki kutoka nchini Marekani Mariah Carey ameamua kuahirisha kutumbuiza katika onesho lake ambalo lilipangwa kufanyika mjini Hawaii kwa kuhofia maambukizi ya virusi hatari vya Corona ambavyo vimeanza kutishia na kuenea nchini Marekani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Carey ametoa taarifa na kuwaomba radhi mashabiki wake wa mjini Honolulu kuwa anaahirisha onesho lake hilo ambalo lilitarajiwa kufanyika March 10 mwaka huu.

https://www.instagram.com/p/B9Sg_t4p690/

“Aloha Hawaii……! Kwa masikitiko makubwa nachukua fursa hii kuwatangazia mashabiki zangu kwamba nimeamua kuahirisha show yangu hadi Novemba mwaka huu. Nilikuwa na furaha kubwa sana kuja Hawaii ukiwa ni mwezi wangu wa kumbukumbu lakini kutokana na masharti yaliyowekwa kwenye usafiri wa Kimataifa, umetulazimu kila mmoja kufikiria juu ya Usalama na Ustawi kwa sitoweza kufanya show yangu tena hadi hapo mwezi Novemba”

Mbali na Mariah Carey wasanii wengine walioahirisha show zao ni Mwimbaji wa R & B kutoka Marekani na mtunzi wa nyimbo Khalid, pamoja, kundi la muziki la Kikorean pop group (BTS), bendi ya Kimarekani ya US Day Green na msanii wa Kifaransa Avril Lavigne pia wameahirisha Tamasha lao na kutarajiwa kutangaza  tarehe ya tamasha lao linalotarajiwa kufanyika huko barani Asia.

Wengine ni Rapper Stormzy kutoka  Uingereza ambaye alitarajiwa kufanya show Malaysia, Singapore, Japan, Uchina na Korea Kusini katika wiki zijazo lakini ameamua kuahirisha  maonyesho yake hadi baadaye ingawa anatarajiwa kuyafanya ndani ya  mwaka huu. Aliwaambia mashabiki: ‘Nilitarajia sana kuuleta ulimwengu pamoja katika tour yangu ya barani Asia lakini kwa sababu ya wasiwasi unaoendelea wa kiafya kutokana na kusambaa kwa Coronavirus, ninahuzunishwa sana na naamini tutakutana tena pale mambo yatakapokuwa mazuri. ‘ Aliongezea: ‘Ninaahidi nitarudi.’

Mbali na hilo Pia kuna wasiwasi kwa wapenzi wa muziki nchini Uingereza virusi vya Corona vinaweza kulisimamisha Tamasha la siku tano la Glastonbury mwishoni mwa mwezi Juni, ambapo watu 200,000 inatarajiwa kuhudhuria tamasha hilo. Pia mnda mkubwa wa vitabu unaofanyikaga jijini London  “London Book Fair ” uliotarajiwa kufanyika  wiki ijayo, uliotarajiwa kuhudhuriwa na mamia ya waandishi mashuhuri na maelfu ya mashabiki wao, ukifutwa mapema hivi leo.

 

https://www.instagram.com/p/B9WRPhFho3h/

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents