Habari

Vyombo vya Habari vilivyoandika habari za ‘KICHOCHEZI’ kupatiwa tuzo za mwaka

Kama umekuwa mfuatiliaji wa vyombo vya habari vya kimataifa kama CNN, Al Jazeera, BBC, FOX na vituo vingine vikubwa bila shaka ulishawahi kukuTAna na taarifa za Rais wa Marekani, Donald Trump akivilaumu vyombo kadhaa vya habari kuwa vinamchafua yeye na Marekani kwa kuandika habari za uwongo.

Sasa taarifa ni kwamba Rais Trump leo Januari 13, 2018 ametangaza kutoa tuzo kwa vyombo hivyo ambavyo amekuwa akivituhumu tangu aingie madarakani.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Trump amesema atatangaza washindi wa tuzo hizo Jumatatu ijayo ambapo vigezo vyake amevitaja kuwa ni vile vyombo vya habari vilivyoandika Habari za Uwongo, kuripoti matukio yenye lengo la kuvuruga amani ya Marekani na vyombo vilivyoongoza kupokea rushwa ili kupika habari.

Hata hivyo tamko hilo ni msisitizo wa tamko lake la awali alilotoa mwezi Novemba mwaka jana ambapo alisema kituo cha CNN kinastahili tuzo ya kituo kinachorusha habari za Uwongo (Fake News).

Soma zaidi – Rais Donald Trump awashambulia CNN, adai wanamchafua yeye na Marekani

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents