Habari

Wabunge wa Uruguay waupitisha muswada wa kuhalalisha matumizi ya bangi

Kama muswada utapitishwa na baraza la senate, Uruguay itakuwa nchi ya kwanza kuratibu uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa bangi. Uamuzi huo unaungwa mkono na serikali ya Jose Mujica, anayesema kuwa itaondoa faida kwa wauzaji haramu wa majani hayo.

Rolling_Joint4

Katika muswada huo, ni serikali tu ndio itaruhusiwa kuuza bangi. Wanunuaji watatakiwa kujiandikisha kwenye database maalum na watatakiwa kuwa zaidi ya miaka 18. Watakuwa na uwezo wa kununua hadi gram 40 kwa mwezi kwenye maduka maalum ya madawa au kupanda mimea sita nyumbani kwao.Hata hivyo, sheria hiyo haiwahusu raia wa kigeni.

Muswada huo uliungwa mkono na wabunge 50 kati ya 96 baada ya mdahalo mzito wa masaa 13 kwenye mji mkuu, Montevideo. Watu wanaounga mkono hatua hiyo wanadai kuwa mapambano dhidi ya madawa ya kulevya yameshindikana hivyo nchi hiyo inahitaji mbinu mpya.

Rais Mujica anasema hawajawahi kuvuta bangi lakini anaamini haitakiwi kuwa haramu. Kwa sasa muswada huo unasubiri kupitishwa na baraza la Senate, ambako serikali hiyo ya mrengo wa kushoto ina watu wengi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents