Habari

Wafanyakazi wawili wa zamani wa Azam ICD watupwa jela miaka 315

Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, imewahakumu wafanyakazi wawili wa zamani wa Bandari Kavu ya Azam ICD, kutumikia kifungo cha miaka 315 jela, baada ya kupatikana na hatia ya makosa ya 105 ya kughushi na moja la kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 12.7 kwa makosa ya kutakatisha fedha na kukwepa kodi.

Raymond Adolf Louis wa kwanza kushoto mwenye shati Jeupe,  Khalid Yusufu Louis  wa kati kati 

Mbali na kifungo hicho, mahakama imewaamuru washtakiwa hao baada ya kumaliza kifungo chao kulipa fidia ya TSh. bilioni 6.35 sawa na nusu ya fedha waliyoisababishia hasara Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya TSh. bilioni 12.7 .


Hukumu hiyo ilitolewa jana na Jaji Winfrida Korosso na kuwataja washtakiwa waliotiwa hatiani kuwa ni Malembo, Meneja wa Operesheni za Usalama Azam, Raymond Louis na mfanyakazi wa Azam, Khalid Yusufu Louis.


Katika kesi ya msingi, washtakiwa walikuwa wakikabiliwa na mashtaka 110 ikiwamo ya kula njama, utakatishaji wa fedha na kukwepa kodi.
Jaji Korosso amesema washtakiwa Raymond na Khalid wametiwa hatiani kwa mashtaka ya kughushi la pili hadi la 106.


Mahakama yangu inawatia hatiani na kuwahukumu Raymond na Khalid kwenda jela kutumikia kifungo cha miaka mitatu kila kosa kwa kosa la pili mpaka la 106, pia watatumikia kifungo cha miaka miwili kwa kosa la kuisababishia hasara TRA pamoja na Malembo,“amesema Jaji Korosso.


Jaji Korosso, baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi 34 bila kuacha shaka, mahakama imewakuta na hatia na kuwahukumu adhabu hiyo.


Hata hivyo, mahakama hiyo imewaachia huru washtakiwa wawili waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka hayo baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao.


Washtakiwa walioachiwa ni, Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Biashara TRA, Hamis Omary, Haroun Mpande wa kitengo cha mawasiliano na kompyuta ICT TRA.


Jaji Korosso alisema amepitia maelezo ya upande wa mashtaka na yale ya washtakiwa pamoja na mawakili wa utetezi na kusema washtakiwa ni wakosaji wa kwanza na kwamba wanafamilia zinazowategemea kwa kuwa wote wana wake na watoto ambao wanawategemea.


Jaji alisema, amezingatia maombi yote ya washtakiwa kuwa wanajutia makosa yao na pia mshtakiwa Raymond na Khalid, wameiomba mahakama iangalie kipindi cha zaidi ya miaka mitatu walichokaa gerezani.


Katika kesi ya msingi Raymond na Khalid wanadaiwa kutoa makontena kwenye Bandari Kavu ya Azam ICD iliyopo maeneo Sokota na kujaribu kuonyesha yalitolewa kihalali na TRA Dar es Salaam huku wakijua walighushi.


Shtaka lingine wanadaiwa kulisababisha hasara taifa ya TSh. 12, 618,970,229 kwa kutoa makontena 329 bila ya kulipia ushuru na malipo mengine.

Chanzo: Nipashe- https://www.ippmedia.com/sw/habari/mahakama-ya-mafisadi-yahukumu-2-miaka-315

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents