Habari

Wafungwa wauwawa kwa risasi wakijaribu kutoroka

Maafisa wa magereza nchini Papua New Guinea, wamewapiga risasi na kuwauwa wafungwa wapatao 17,waliovunja gereza wakijaribu kutoroka siku ya Ijumaa.

Polisi wamewatia mbaroni wafungwa watatu, huku wakiendelea kuwasaka wengine 57 ambao bado hawajulikani waliko tangu kutokea kwa kisa hicho katika gereza la Buimo, katika mji wa Lae. Idara ya usalama nchini humo imewatahadharisha raia wa nchi hiyo kuwa macho na watoe taarifa kwa vyombo vya usalama pindi wakiwaona wafungwa hao.

Polisi wanasema kuwa, wengi wa wafungwa waliotoroka walikuwa wahalifu sugu.Gereza hilo la Buimo huwa na msongamano mkubwa wa wafungwa kikikadiriwa kuwa na wafungwa 400 katika mwezi febuari pekee. Mwaka 2016 wafungwa 12 waliuawa baada ya kujaribu kutoroka katika gereza hilo.

Kwa mujibu wa kituo cha television cha EMTV, Gereza la Papua New Guinea ni gereza la pili linaloongoza kuwa na wahalifu wengi duniani.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents