Technology

Kirusi kinahofiwa kujitokeza Kwenye kompyuta leo

Wataalmu wa usalama ya mitandao katika komputa, wanaonya kwamba kunaweza kutokea mashambulio mengine katika baadhi ya miji dunia, pale tu wataporudi makazini siku ya leo.

inasadikika kuwa komputa zaidi ya 120 katika nchi kama 100, zilidukuliwa siku ya Ijumaa.Lakini polisi wa Umoja wa Ulaya wanasema walioathirika ni 200,000 katika nchi 150.

Shambulio hilo limeathiri watumiaji wakiwemo ofisi za serikali, kampuni zinazotengeneza magari, mabenki na huduma za afya.Hata hivyo kampuni ya Microsoft imesema kuwa tukio hilo ni kama funzo.

Taarifa kutoka kwa rais wa Microsoft na afisa mkuu wa maswala ya sheria Brad Smith siku ya Jumapili ilikosoa vile serikali zinavyoweka taarifa zao kuhusu dosari za kiusalama katika mifumo ya kompyuta.

‘Tumeona dosari zinazohifadhiwa na CIA zinaonekana katika Wikileaks na sasa dosari ilioibwa kutoka kwa NSA imeathiri wateja kote duniani’a ‘, aliandika Microsoft.

Kirusi hicho kilichojitokeza wiki iliyopita kiliweka dosari kwenye toleo la programu ya Microsoft Windows ambacho kilikuja kugunduliwa na majasusi wa Marekani.

Kwa sasa Kampuni nyingi zimeajiri wataalam waliofanya kazi wikendi kuzuia maambukizi mapya.Japo kuna hofu ya kirusi kipya kujitokeza siku ya leo.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents