FahamuHabariTechnology

Teknolojia ya AI itaathiri ajira za watu kwa asilimia 40 duniani – IMF

Teknolojia ya Artificial Intelligence (AI) kwa Kiswahili Akili Mnemba inatarajiwa kuathiri karibu 40% ya kazi za watu mbalimbali kulingana na uchambuzi mpya wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

Mkurugenzi mkuu wa IMF Kristalina Georgieva anasema “katika hali nyingi, AI itazidisha ukosefu wa usawa kwa ujumla”.

Bi Georgieva anaongeza kuwa watunga sera wanapaswa kushughulikia “mwenendo unaosumbua” ili “kuzuia teknolojia dhidi ya kuchochea zaidi mivutano ya kijamii”.

Kuenea kwa AI kumeweka faida na hatari zake chini ya uangalizi.

IMF ilisema AI itaathiri idadi kubwa ya ajira – ikiwa ni karibu 60% – katika uchumi wa juu.Katika nusu ya matukio haya, wafanyakazi wanaweza kutarajia kufaidika kutokana na ushirikiano wa AI, ambayo itaongeza tija yao.

Katika hali nyingine, AI itakuwa na uwezo wa kufanya kazi muhimu ambazo kwa sasa zinatekelezwa na wanadamu.Hii inaweza kupunguza mahitaji ya wafanyikazi, kuathiri mishahara na hata kumaliza kazi.

Wakati huo huo, IMF inakadiria kuwa teknolojia hiyo itaathiri asilimia 26 tu ya nafasi za kazi katika nchi zenye kipato cha chini.

Bi Georgieva alisema “nyingi za nchi hizi hazina miundombinu au nguvu kazi yenye ujuzi kutumia manufaa ya AI, na hivyo kuongeza hatari kwamba baada ya muda teknolojia inaweza kuzidisha ukosefu wa usawa kati ya mataifa”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents