Habari

Mwanafunzi kidato cha pili ashikiliwa na polisi kwa tuhuma za mauaji

Watu watano akiwemo mwanafunzi wa kidato cha pili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya vikongwe wawili yaliotokea wilayani Sengerema mkoani Mwanza mwaka jana.

Ambao wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya Sophia Maduka,(61) na Mathias Lusesa,(73) wote wakulima na wakazi wa Lwenge Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habar Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa ameeleza kuwa mnamo Oktoba 12,2023 majira ya saa mbili (20:00) usiku katika Kijiji cha Lwenge Kata ya Kagunga Wilaya ya Sengerema watu wawili waliuawa kwa kukatwa na vitu vyenye ncha kali sehemu mbalimbali za miili yao.

Mutafungwa ameeleza kuwa baada ya taarifa hiyo kuripotiwa kituo cha polisi,jeshi hilo lilifanya msako mkali na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao waliokuwa wamejificha kukwepa mkono wa sheria.

Ambapo Januari 06,2024 kwa nyakati tofauti na maeneo tofauti katika Mkoa wa Geita na Shinyanga Askari wa upelelezi kutoka Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na Askari wa mikoa hiyo jirani walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao watano.

Mutafungwa amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Selina Mchele(48),mkulima na mkazi wa Kijiji cha Mwakilemwa,Maneno Mashauri,(19)mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Lwenge Wilaya ya Sengerema, Majaliwa Damas,(22) Mganga wa tiba asilia,mkazi wa Masumbwe mkoani Geita, Ntingwa Kilimanjaro kwa jina maarufu Shetani(42)mkulima na mkazi wa Kijiji cha Mbamba mkoani Geita na Emmanuel Damas,(34),Mganga wa tiba asilia,mkazi wa Kijiji cha Burungwa mkoani Shinyanga.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents