HabariSiasa

Wahamiaji haramu wanaoingia Uingereza kuhamishiwa makazi Rwanda

Uingereza imeingia kwenye makubaliano na Rwanda, ambayo sasa itaanza kuwapokea wahamiaji haramu wanaoingia katika taifa hilo la Ulaya.

Katika makubaliano hayo yaliyotiwa saini jijini Kigali, serikali ya Rwanda itapokea malipo ya awali ya Dola Milioni 157 ili kufanikisha mpango huo na kuwapa hifadhi wahamiaji hao.

Waziri Mkuu wa Uingereza, akizungumzia makubaliano hayo, amesema hatua hii itasaidia kupunguza idadi ya wahamiaji haramu wanaoingai nchini humo kupitia usafiri wa majini.

Rwanda imekaribisha ushirikiano huu ambao inasema, itatoa nafasi kwa wahamiaji hao kupata msaada na watajumuishwa katika jamii, lakini kama taifa itanufaika pia.

Vincent Biruta ni Waziri wa Mambo ya nje wa Rwanda amezungumzia mpangu huu baada ya kutiliana saini na Waziri wa Mambo ya ndani wa Uingereza Priti Patel.

Haitakuwa mara ya kwanza kwa Rwanda kupokea wakimbizi, miaka miwili iliyopita, ilianza kuwapokea mamia ya wakimbizi kutoka Libya, na mpango huu unakuja licha ya kukosolewa na watetezi wa haki za binadamu.

Baadhi ya wanasiasa wa upinzani wamepinga mpango huu wa Uingereza wakisema, ni ukiukwaji wa haki za binadamu, licha ya serikali nchini humo kupata shinikizo za kuzuia maelfu ya wahamiaji haramu.

Wasiwasi kama huo pia unatolewa na watetezi wa haki za binadamu wanaosema huenda wahamiaji watakaopelekwa Rwanda haki zao zikakiukwa kwa sababu ya nchi hiyo ya Afrika ya Kati kutokuwa na historia nzuri ya kuheshimu haki za binadamu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents