Habari

Wahitimu NIT watakiwa kutumia ujuzi wao kuwanufaisha watanzania

WAKATI sekta ya usafirishaji ikitajwa kuwa ndiò msingi wa maendeleo endelevu nchini, wahitimu wa mafunzo ya umahili katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wametakiwa kuhakikisha ujuzi walioupata unawanufaisha watanzania.

Hayo yalibainishwa jijini Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (UDART), Gilliard Ngewe wakati wa kongamano la 10 la Wahitimu wa Chuo NIT lililokwenda sambamba na utoaji wa zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri kwenye vitivo mbalimbali vya chuo hicho.

Ngewe alisema wahitimu hao wamepatiwa ujuzi wa kutosha hivyo ni wakati wao sasa kwenda kuutumia kwa jamii kwa kuhakikiha sekta ya usafirishaji inakuwa salama na yenye kuwanufaisha watanzania wote kwa ujumla.

“Leo wahitimu wa NIT waliofanya vizuri katika masomo yao wamepewa zawadi ili wapate motisha huko wanapokwenda wakatoe huduma za usafirishaji hasa zile ambazo zitawanufaisha Watanzania wote, hata hivyo ni muhimu mkafuate sheria ili abiria na vyombo viwe salama,” alisema

Hata hivyo alisema kuwa mchango wa NIT kwenye sekta hiyo ya usafirishaji ni mkubwa na kwamba unalisaidia taifa katika kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

Naye Kaimu Mkuu wa chuo cha NIT Zainabu Mshana alisema kuwa chuo hicho kinajivunia kutoa wataalam wengi ambao wataokwenda kutoa suluhisho la usafiri nchini.

“Mwaka jana walihitimu wanafunzi 2700 lakini mwaka huu wamehitimu wanafunzi 3600 tunajuvunia kutoa wataalam waliopata mafunzo ya umahili kwa lengo kutatua changamoto za usafiri” alisema.

Aidha Mshana alisema kuwa wanafunzi hao watakuwa chachu ya maendeleo kwa kuwa sekta hiyo ndio msingi wa maendeleo hapa nchini

“Kupitia ujuzi wao watatuletea maendeleo endelevu kwa kuwa usafirishaji ndio msingi wa maendeleo” alisema.

Bariki Seme ni Mhitimu wa Stashahada katika ukarabati wa Meli alisema kuwa amefurahi kuhitimu mafunzo hayo na kwa kuwa nchi ina malengo ya kujikita kwenye uchumi wa Buluu basi atatoa mchango wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents