Michezo

Wakati umefika kwa klabu kuthamini jezi zao – Tarimba (Video)

Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara klabu ya Dar es salaam Young Africans imezindua jezi zao ambazo kwa mara ya kwanza wakiwa chini ya mdhamini wao mkuu kampuni ya kubashiri matokeo ya Sportpesa.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji ndugu Tarimba Abbas alisema “Sportpesa ni kampuni ambayo lengo lake kuu ni kuendeleza na kuinua vipaji vya michezo hasa mpira wa miguu nchini Tanzania” alisema Tarimba Abbas

Abbas ameongeza kuwa “Leo tunaendeleza ile adhima yetu ya kuwa na mahusiano mazuri na klabu hizi tatu Singida United, Simba SC na Yanga SC katika utaratibu wa kuwapatia vifaa na hasa jezi pamoja na vitendea kazi vingine ambavyo watavitumia katika mashindano yanayokuja msimu huu.

Hivi leo ni zamu ya Young Africans tutawakabidhi rasmi jezi ambazo zitatumika huku zikiwa na nembo ya Sportpesa.

Mkurugenzi huyo wa kampuni ya Sportpesa ameonyesha kukerwa na kitendo cha jezi za Yanga kuzinduliwa bila utaratibu huku kukifanyika mzaha katika hafla hiyo “Kuna jambo tungependa tulizungumze ambalo kusema kweli limetokea hivi majuzi ambalo hatukufurahi nalo kabisa pale ambapo jezi zilizotolewa kwa minajali ya kwenda kufanyiwa printing ghafla tunaziona katika sherehe ambayo jezi zile hazikutoka huko na pakawa na mzaha”.

“Wakati umefika kwa klabu zetu za Tanzania kuthamini jezi zao kwasababu zinatumika kibiashara, hivi ninavyozungumza ukitoka nje hapa utakuta kwenyemiti zimetundikwa zinauzwa tena mbaya zaidi zinamajina hata ya wachezaji wa sasa hivi  walio sajiliwa na Yanga”.

Akiongea kwa niaba ya uongozi wa Young Africans Sports Club, Mjumbe wa kamati ya Utendaji, Salum Mkemi alianza “kwa kushukuru kampuni ya Sportpesa kwa ushirikiano wao kuanzia kuwaletea mashabiki wengi timu hiyo, kuwatangza kwenye vyombo mbali mbali vya habari na uongozi wa Yanga unajivunia kuwa moja kati ya washirika wa Sportpesa”

Katika mchezo huo wa kirafiki uliyo wakutanisha mabingwa watetezi klabu ya Yanga dhidi ya Singida umemaliza kwa wanajangwani kuchomoza na ushindi wa magoli matatu kwa mawili dhidi ya wageni wa ligi kuu Singida United.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents