Michezo

Tunashukuru Sportpesa kwa kutujali – Paralympic Committee (TPC) (Video)

Kamati ya michezo kwa watu wenyeulemavu nchini imeishukuru kampuni ya kubashiri matokeo Sportpesa kwa kuonyesha kuguswa na watu wenye ulemavu, hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Tanzania Paralympic Committee(TPC), Tuma Dandi alipozungumza na Bongo5 wakati walipotembelewa na mchezaji wa zamani wa Arsenal, So Campbell katika uwanja wa Karume uliyopo ofisi za TFF Jijini Dar es laam

Mchezaji wa zamani wa Arsenal, So Campbell(kushoto) akiwa na Katibu Mkuu wa Tanzania Paralympic Committee, Tuma Dandi (kulia) wakifurahia jambo

“Tupo hapa kwaajili ya kukubali wito wa Sportpesa ambao wameona michezo ya watu wenye ulemavu imeachwa nyuma watu wanaweza wakawa wanajua lakini hawaithamini haina wafadhili kwa sababu mbalimbali” alisema Tuma Dandi Katibu Mkuu wa Tanzania Paralympic Committee .

Dandi ameongeza kuwa “Kwa hiyo tunawashukuru sana Sportpesa ambao wameonyesha kuguswa na michezo yetu ya watu wenye ulemavu”.

Kwa upande wake kocha wa timu ya walemavu ya Muungano, Zaharani Seleman Mwenemti amesema “Sisi shukrani zetu za dhati tunawapelekea Sportpesa kwa hili swala walilojitolea kuiyona jamii hii yenye mahitaji maalum nayo ishiriki katika swala zima la michezo”, alisema Zaharani Seleman kacha wa timu hiyo.

“Kama unavyojua ulemavu sikushindwa moja kwa moja kama unavyoona hapa  zipo tomu mbili ni mchezo wa ushindani tu, kwa hiyo Sportpesa wameanza nawengine wajitokeze katika swala zima la kutoa mchango wao katika timu za walemavu”.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents