Habari

Waliofariki MV Nyerere wafikia 151 , Mbunge wa Ukerewe adai changamoto za kivuko zilitatuliwa

Wakati idadi ya watu waliofariki dunia katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama juzi mchana Septemba 20, 2018 imefikia 151 huku uokoaji ukiendelea, Mbunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi amesema kivuko hicho kilifanyiwa ukarabati kama alivyoomba bungeni.

Toka itokee ajali hiyo video ya mbunge huyo akiwa bungeni kuomba kikarabitiwe kivuko hiko, imekuwa ikisambaa mitandaoni na kuzua hisia tofauti. Amesema kuwa Kivuko hicho kilifanyiwa ukarabati miezi miwili iliyopita, hivyo kilikuwa sawa na kilikuwa mbioni kubadilishiwa ratiba ikiwemo kuongeza idadi ya safari ili kukidhi mahitaji ya wananchi wa eneo hilo. “Kuhusu hoja yangu niliyoitoa bungeni, ilifanyiwa kazi ambapo tulikuwa tunahitaji injini mbili ambazo zilipatikana na zikafungwa labda tu suala ambalo lilikuwa bado tunalifanyia kazi ni kuona namna gani tunaweza kubadilisha idadi ya safari”, amesema Mkundi Akiwa kwenye eneo la tukio leo, Mtangazaji wa TBC1 Enock Bwigane amesema ameona miili 15 ikiwa inaopolewa. Jana, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipowasili katika Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe alisema idadi ya waliokufa kwenye ajali hiyo ilikuwa watu 136 hivyo pamoja na iliyoopolewa leo inafanya idadi ya walioopolewa kufikia 151.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents