Habari

Wanafunzi 11 wafariki shule ikiungua moto Uganda

Takriban wanafunzi 11 wamekufa na wengine sita wako katika hali mbaya baada ya moto kuzuka katika shule ya walemavu wa macho katikati mwa Uganda.

Polisi ya Uganda imesema moto ulitokea saa saba usiku wa kuamkia jana katika shule ya Salaama, iliyoko Mukono, takriban kilomita 30 mashariki mwa mji mkuu Kampala.

Polisi imeendelea kueleza kuwa chanzo cha moto huo bado hakijajulikana. Mara nyingi matukio ya moto hutokea katika shule za mabweni nchini Uganda, na aghalabu hulaumiwa kwa makosa ya uunganishaji wa nyaya za umeme. Lakini mamlaka inasema baadhi ya matukio hayo huanzishwa kwa makusudi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents