Habari

Warembo wamtosa Dj Choka kwenye video ya ‘Pamoja we Can’


Jumapili hii Dj maarufu na mmiliki wa blog ya muziki Dj Choka alikuwa anashoot video ya wimbo wake mpya aliowashirikisha wasanii zaidi ya saba, ‘Pamoja we Can’.
Shughuli nzima ya uchukuaji wa video hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa New Maisha Club.
Awali Dj Choka alikuwa ametumia sana ukurusa wake wa Facebook na Twitter kuwaomba akinadada kujitokeza kwa wingi ili kumuunga mkono kwa kuonekana kwenye kichupa hicho.

Tofauti na matarajio yake, Dj Choka, alijikuta akichoka kama jina lake lilivyo baada ya ukumbi mzima kuona umejaa wanaume tu, hakuna msichana hata mmoja!
Kuona hivyo ilibidi avute subira kwanza labda watotokea warembo kadhaa ili mpango mzima wa kushoot video uanze.
Hata hivyo pamoja na kukatishwa tamaa na mahudhurio zero ya akinadada licha ya kuwaomba wafanye hivyo, shughuli ilibidi iendelee na kushirikisha midume tupu.

Miongoni mwa wasanii watakaonekana kwenye video hiyo ambao wengi wao wameshiriki kwenye wimbo huo ni pamoja na Baghdad, Cyrill, Deddy, Dj Choka mwenyewe, Mabeste, Noorah, Producer Pancho, Shetta, Stereo, Young Deen na wengine.
Pengine Dj huyu anatakiwa kubadilisha mfumo wa kutafuta video models kwa kutumia status za Facebook, na badala yake aandae bajeti ya kutosha ili awatafute yeye mwenyewe walipo kwa makubaliano maalum. Video ain’t cheap bro! The better the video the bigger the budget.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents