Burudani

Wasanii waanzisha tamasha la kumuenzi baba wa taifa, Mwana Fa atoa ya moyoni “Baba wa taifa amesahaulika sio kama akina Mandela” – Video

Wasanii waanzisha tamasha la kumuenzi baba wa taifa, Mwana Fa atoa ya moyoni "Baba wa taifa amesahaulika sio kama akina Mandela" - Video

Tamasha la kumuenzi baba wa taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere ambalo limeanzishwa na wasaniii wote nchini likizinduliwa leo katika ukumbi wa Mwl nyerere Conferece Center Posta Jijini Dar Es Salaam,maadhimisho haya yakitarajiwa kuambatana na shughuli mbalimbali zinazofanywa na Serikali, vikundi na watu binafsi, lengo kubwa ni kumkumbuka mwasisi wa taifa letu kutokana na kujitoa kwa kila namna dhidi ya utawala dhalimu wa kikoloni na hatimaye kuleta uhuru ambao tunajivunia kwa kuupata bila kumwaga damu.

Katika uzinduzi ulifanyika katika ofisi za bodi ya filamu Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na mjumbe wa bodi ya Baraza la Sanaa Taifa BASATA ameeleza jinsi anavyojisikia vibaya kuona hakuna matukio makubwa yanayomhusu baba wa taifa kwani alisaidia mataifa mengi barani Afrika kupata uhuru lakini watu kama Nelson Mandela ambao yeye aliwasaidia wao wana matukio mengi ya kuonyesha upenda kwa kulikombo taifa lao lakini kwa baba wa taifa amekuwa kama amesahaulika.

Ikumbukwe Tamsha mpya la Mwl Nyerere Festival linalotarajiwa kuzinduliwa leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Tamasha hili likianzishwa na wasanii wa Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents