Burudani

Wasanii waliofanikiwa kimataifa wawe tayari kuwapa wengine ‘connection’ – Bayo

Rapper na msanii wa dancehall, Bayo amekiri kuwa muziki wa Tanzania umefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika jukwaa la kimataifa lakini ametaka wasanii waliotangulia kuwa tayari kuwaonesha njia wasanii wengine pia.

Bayo ambaye pia ni mfanyakazi wa taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na masuala ya vijana visiwani Zanzibar amesema kwa kufanya hivyo Tanzania itakuwa na wawakilishi wengi zaidi kimataifa.

“Hakuna kitu kikubwa kama connection au network, kama hawa watu wanaotoboa wawe willing pia kushare – japo sometimes huwezi kuuza ramani yako yote sababu vitu vingine mtu anaona kabisa hii ni hustle yangu halafu nimpe mtu kiulani tu na yeye apite mule mule haiwezekani,” amesema Bayo.

Hata hivyo Bayo amesema ni muhimu utamaduni wa kushirikishana ukawepo ili wasanii wengi zaidi waweza kufanikiwa.

Bayo anatarajia kuachia wimbo wake mpya uitwao ‘Kitimtim.’

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents