HabariUncategorized

Wapenzi wanaoishi bila kufunga ndoa kuadhibiwa vikali

Serikali nchini Burundi imesema imejiandaa vya kutosha kuwachukulia hatua za kisheria watu ambao wanaishi kwenye mahusiano kama mume na mke bila kufunga ndoa na wale wanaoishi kwenye ndoa bila kusajili ndoa zao serikalini.

Kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani nchini Burundi, Serikali imesema imeanza kukusanya ripoti ya watu wanaoishi pamoja kama wapenzi ambao hawajafunga ndoa au kutokusajili rasmi ndoa zao serikalini ili kuwabaini wote waliokiuka amri ya serikali iliyotolewa mwaka jana ikiwataka wananchi wote nchini humo kusajili ndoa zao kabla ya Desemba 31, 2017.

Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza jana kwenye taarifa yake aliyoitoa kupitia kituo cha taifa cha Radio cha Burundi cha RTNB amewaonya vikali watu wote waliokiuka amri hiyo ya serikali na kuahidi kuwa sheria itachukua mkondo wake bila kujali sababu za kidini.

Kwanza tunashukuru watu wote waliokuja kusajili ndoa zao serikalini kwa sasa watu ambao wamekaidi amri hiyo sheria itafuata mkondo wake, jambo lingine tumegundua tunajenga hoja za dini au madhehebu na kukaidi amri hiyo, dini haiwezi kuwa mpinzani wa sheria hatua hii itatusaidi kuzuia ongezeko la watu, maana yake leo hii ukiwa na wanawake watano utajikuta unakuwa na watoto 20 na sio tu wanakuwa hawatambuliwi kisheria lakini pia wanaleta shida nchini.“amesema Pierre Nkurunziza.

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2017 kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani nchini Burundi, watu 166,000 wanaishi nje ya ndoa.

Hatua hiyo imepingwa vikali na wanaharakati nchini humo pamoja na waislamu  ambao hao kwa sheria za dini yao wanaruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja ile hali amri ya serikali inakataza.

Chanzo : Jeune Afrique

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents