Burudani

Watanzania tuchape kazi kwelikweli kwa sababu hakuna cha bure – Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amewataka Watanzania kufanya kazi kwa bidii kama ilivyokuwa kwa Yesu Kristo ambaye alikuwa chini ya malezi ya fundi seremala.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli

Rais Magufuli ametoa rai hiyo leo (jana) katika Kanisa la Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu mjini Singida katika kuadhimisha Sikukuu ya Krismasi ambayo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo.

“Katika kipindi cha maisha yake Yesu Kristo hapa duniani, mbali ya kwamba alizaliwa na mfanyakazi, Joseph seremala, lakini na yeye alishiriki katika kufanya kazi, basi niwaombe watanzania wote tuchape kazi kwelikweli kwa sababu hakuna cha bure,” alisema Rais Magufuli.

Pia amewataka watanzania kuimarisha upendo, kuvumiliana, na kutobaguana, kwani upendo utalisaidia taifa kupata maendeleo huku akiwakumbusha waumini kuwa Yesu Kristo hakuwa CHADEMA wala CCM bali alikuwa ni wa watu wote.

Rais Magufuli ambaye aliambatana na mkewe Mama Janeth Magufuli, katika ibada hiyo amesema, kusali ni moja ya nguzo muhimu ambayo Wakristo wote wanapaswa kutekeleza ili kuhakikisha taifa linaendelea kubakia katika hali ya amani na utulivu ambayo ndiyo msingi wa maendeleo.

Aidha, Rais Magufuli ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wakulima kote nchini kuhakikisha wanazitumia vizuri mvua za sasa katika shughuli za kilimo pamoja na kulima mazao yanayostahimili ukame.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents