Habari

Watu tisa wafariki dunia 23 wajeruhiwa, Ajali ya magari matatu Morogoro (+ Video)

Watu Tisa wamefariki dunia huku wengine 23 kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka katika eneo la Oil Com Manispaa ya Morogoro.

Ajali hiyo imehusisha magari matatu gari la Abiria Toyota Coster yenye namba za usajiri T686 DUK, iliyokuwa ikitokea Dar es salaam kuelekea Mbeya, Gari ndogo aina ya Crester yanye namba za usajili T563 ASA pamoja na Lori la Mizigo kampuni ya Dangote.

Kaimu mganga mfawidhi hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro, Dr Messy Ngarawa na majeruhi Frank Ramson wameelezea kuhusiana na ajali hiyo pamoja na idadi ya vifo na majeruhi.

Bofya hapa chini kutazama.

 

https://www.instagram.com/p/CQarqOjBnXM/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents