Siasa

DC Morogoro Msando, aanza kazi na tukio la ajali ya magari matatu usiku (+ Video)

Baada ya kuapishwa siku ya jana majira ya asubuhi Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando ameanza kazi mara moja baada ya kutokea ajali ya magari kadhaa ambayo imepelekea watu watano kufariki dunia ambapo ajali hiyo imetokea eneo la nanenane mkoani Morogoro ambayo ilihusisha magari matatu ambayo ni Basi dogo aina ya Toyota Coaster, Lori na gari dogo aina ya Toyota Cresta.

Mbali na Kamanda wa Polisi Morogoro Fortunatus Muslim kueleza chanzo cha ajali hiyo ambapo alisema kuwa ni uzembe wa Dereva wa Coaster kutaka kuyapita magari yaliyopo mbele yake bila kuchukua tahadhari akitokea Dar es salaam kuelekea Mbeya kuzika ikiwa amebeba mwili wa Marehemu pamoja na Abiria.

Pia Mkuu wa Wilaya hiyo Albert Msando alifika eneo la Tukio na kufanikiwa kuzungumza na wana habari na kueleza haya yafuatayo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents