Habari

Waziri Mwijage awapongeza Azania Bank kwa kuanzisha kliniki ya biashara(Picha)

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akitoa hotuba kwa wageni waalikwa wakati wa wa uzinduzi wa Kliniki ya Biashara ambayo itatoa huduma za ushauri wa masuala ya kibiashara katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kliniki ya Biashara ambayo itatoa huduma za ushauri wa masuala ya kibiashara katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam, mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo Charles Itembe alisema lengo la benki hiyo ni kutoa huduma za kifedha kwa wazalishaji bidhaa, viwanda pamoja wakulima kwa ajili ya kusaidia kukuza biashara zao.

Kliniki hiyo ambayo itatoa huduma zote za ushauri wa masuala ya kibiashara sehemu moja, imeundwa na mamlaka ya Kuendeleza Biashara Tanzania (TANTRADE)

Ikiwa na kauli mbiu “Kusaidia Maendeleo Endelevu na ukuaji wa Biashara”, Kliniki hiyo itakuwa ni ya kwanza na ya aina yake ambayo itatoa ushauri kwa aina mbali mbali za biashara ikiwa ni pamoja na biashara ndogo, za kati na kubwa ambazo zitakuwa zinashirikim katika maonyesho ya Sabasaba

Mkurugenzi huyo alisema benki ya Azania inatoa huduma mbali mbali za kifedha ikiwa ni pamoja na mikopo ya biashara, mikopo binafsi, mikopo ya nyumba na mikopo hiyo hutolewa kwa riba ndogo

“Tunawakaribisha watu wote wanaoshiriki maonyesho ya Sabasaba na wanaokuja kutembea kwenye banda letu kwa ajili ya kupata huduma zan kifedha,” alisema

Alitaja baadhi ya huduma zinazotolewa na benki hiyo ni pamoja na kusaidia bishara za kuuza bidhaa nje ya nchi na kuingiza ndani ya nchi ikiwa ni pamoja na malighafi zinazotumika viwandani, kusaidia wazalishaji na wasindikaji wa bidhaa za kilimo, kusaidia kutoa mitaji ya uendeshaji wa viwanda, kutoa dhamana ya kibenki kwa ajili ya kusaidia miradi ya miundombinu, biashara.

“Tunaamini kupitia mchango wetu wa huduma za kifedha kwenye sekta ya viwanda na kilimo tutakuwa tumeiunga mkono Serikali kufikia lengo kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kufikia mwaka 2025,” alisema

Itembe aliipongeza TANTRADE kwa kufungua Kliniki ya Biashara ambayo itawaleta pamoja wadau mbali mbali wa biashara kutoka sekta binafsi na umma watakao toa majibu kwa changamoto mbali mbali za kibiasaha na kuongeza kuwa benki ya Azania ni moja ya wadau ambao watakuwepo kwenye kliniki hiyo kwa ajili ya kutoa suluhisho na ushauri kuhusiana na mambo mbali mbali ya kibiashara

Maonyesha ya Sabasaba ya mwaka huu ni ya 42 na yanabeba kauli mbiu “Undelezaji wa Biashara kwa Maendeleo ya Viwanda “


Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage na Naibu waziri wa viwanda na biashara Stellah Manyanya wakifungua kitambaa wakati wa uzinduzi wa uzinduzi wa Kliniki ya Biashara ambayo itatoa huduma za ushauri wa masuala ya kibiashara katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.


Mkurungezi mtendaji wa Azania Bank Charles Itembe akitoaa hotuba kwa wageni waalikwa wakati wa wa uzinduzi wa Kliniki ya Biashara ambayo itatoa huduma za ushauri wa masuala ya kibiashara katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya wafanyabiasharaa na wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage wakati wa wa uzinduzi wa Kliniki ya Biashara ambayo itatoa huduma za ushauri wa masuala ya kibiashara katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents