Habari

Waziri wa Mambo ya Nje Lebanon ajiuzulu

Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanon, Nassif Hitti ametangaza kujiuzulu kwake leo akiituhumu serikali kuushughulikia vibaya mzozo wa kiuchumi mbaya zaidi kuwahi kulikumba taifa hilo kwa miongo kadhaa.

Lebanese foreign minister resigns as economic crisis deepens | The ...

Mzozo huo umeipelekea serikali ya Lebanon kuomba msaada kutoka kwa Shirika la Fedha Duniani IMF. Waziri huyo, Nassif Hitti amesema serikali ya Lebanon imeshindwa kutekeleza mabadiliko yanayotakikana na wafadhili wa kimataifa.

Mzozo huo wa kiuchumi ambao ni mbaya zaidi tangu vile vita vya wenyewe kwa wenyewe vya kati ya mwaka 1975-1990 umesababisha mfumko wa bei kuongezaka na bei za bidhaa kupanda jambo linalosababisha umasikini, na maandamano ya raia wenye ghadhabu.

Serikali ya Waziri Mkuu Hasan Diab iliyoundwa mwezi Januari ilisemekana kuwa ni ya wataalam ila imeshindwa kupata uungwaji mkono kimataifa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents