HabariUncategorized

Wema Sepetu alia tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi

Daah! Tukio lililotokea mchana wa Alhamisi hii kwa kupigwa risasi kwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu limewaumiza watu wengi ndani na nje ya Tanzania, miongni mwao ni malkia wa filsamu nchini Wema Sepetu.


Hii ni picha ya gari la Tundu Lissu ambalo limepigwa risasi na mwenyewe akiwemo

Mrembo huyo atakuwa anaumia zaidi kuliko hata watu wengine kutokana na ukaribu wake na Mbunge huyo ambaye wote kwa pamoja wanakitumikia chama cha Chadema na kubwa zaidi ni wakili wake anayesimamia kesi ya madawa ya kulevya inayomkabili muigizaji huyo.

Kupitia mtandao wa Instagram, Wema ameandika:

Kwanza wamuhangaishe kila kukicha kesi haziishi… Akisema kitu uchochezi, sasa kakataa kukaa kimya ndo wameona wamuue…. NO!!! Watanzania kama tutaendelea kufumbia macho huu uonevu then hatutofika tunapotaka… Kero zinazidi kila kukicha… Ndugu zetu wanaonewa kila kukicha… And wat do we do…? Tunakaa Kimya… Jamani kwa hili tuombe tu Mungu huyu baba apone… Nikimaanisha, huko alipo sasa Mungu amsimamie na arudi kwenye hali yake…. Hii sasa imekuwa too much… This is something No One Can Take… Sidhani kama kuna Mtanzania yoyote anaependa hali ya nchi inavyoendelea kuwa kadri siku zinavyozidi kwenda… Ni nini hiki jamani…??? Oh Lord help my Uncle… If anything happens to him then nadhani wengi wetu vitatutokea maana hatutokaa KIMYA…!!! Ni kutokukaa kimya ndo kumepelekea haya yote kutokea… Nimeikumbuka Tanzania yetu ya miaka kama miwili iliopita… Sio Tanzania hii isio na Amani… ???… Nchi gani sijui hii… Mungu tusaidie…!!! I’m Praying for you Uncle wangu…???????

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents