Habari

Wengine watatu kizimbani kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya

Watuhumiwa watatu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoani Pwani wakikabiliwa na mashtaka ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Methemphetamine Kilogramu 424.84 pamoja na Heroin Hydrochloride zenye uzito wa gramu 158.24.

Washtakiwa hao ni Rajabu Kisambwanda (42) mkazi wa Kerege Matumbi, Bakari Said (39) Mkazi wa Kunduchi Mtongani na Hillary Rhite (35) Mkazi wa Kunduchi Sodike.

Wakisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Joyce Mkhoi na Wakili wa Serikali, Agness Ndanzi, alidai mahakamani hapo kuwa, washtakiwa hao watatu walikutwa wakisafirisha dawa hizo za kulevya mnamo tarehe 10 Aprili, 2024 eneo la Zinga wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani .

Wakili Ndazi aliendelea kuieleza Mahakama kuwa, katika tukio lingine, tarehe hiyohiyo mshtakiwa Bakari Said (39) Mkazi wa Kunduchi Mtongani alikutwa akisafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin hydrochloride yenye uzito wa gramu 158.24.

Hata hivyo washtakiwa wote watatu hawakuruhusiwa kujibu chochote kwani Mahakama hiyo haina Mamlaka ya kisheria kusikiliza shauri hilo na watafikishwa tena mahakamani kwa ajili ya kutajwa tarehe 7 mwezi Mei, 2024.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents