Burudani

Weusi hawana mpango wa kusaini wasanii, sababu?

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo kutoka kundi la Weusi, Nikki wa Pili amefunguka sababu za wao kutosaini wasanii.

Weusi

Rapper huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Kihasara’ ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa kuamua kumsaini msanii ni kukubali kubeba ndoto zake zote alizonazo kitu ambacho kwa sasa hawapo tayari.

“Ukisema unafungua label au una kumsaiini mtu, ina maana anakukabidhi ndoto zake mikononi mwako, je unaweza kuzifikisha??, watu wanataka watengeneza maisha yao, sisi tunavyoona bado,” amesema Nikki wa Pili.

“Unamuona Chin Bees tumekuwa naye kitambo kwanini hatukumsaini lakini tumemsaidia mpaka amekuja kupata Wanene. Nikisema sasa hivi namsaini Chin Bees atanidai video kama tatu, atanidai promotion, hiyo itakuwa baadaye one step at a time,” ameongeza.

Nikki wa Pili ameshafanya kolabo tatu na Chin Bees ya kwanza ikiwa ni Role Model, Sweet Mangi na sasa Kihasara.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents