Habari

Will.I.AM wa Black Eyed Peas awakera waingereza kisa kuchat kwenye simu


Waingereza wenye hasira wameuwashambulia uamuzi wa waratibu wa mbio za mwenge wa Olympic nchini Uingereza kumchukua mwanamuziki wa kundi la Black Eyed Peas Will.i.am kuubeba.

Kuchukizwa kwa waingereza hao kumetokana na kitendo cha msaani huyo ambaye pia ni jaji wa mashindano ya kusaka vipaji vya kuimba ya The Voice UK kuwa busy na simu wakati ameushikilia mwenge huo.

[WILL-I-AM akiwa anachat na kutweet kweney simu akiwa amebeba tochi ya Olympic huko Uingereza]

Will.i.am mwenye umri wa miaka 37 na ambaye aliwahi kukiri kuwa addicted na Twitter, alikuwa akitweet muda wote wakati ameubeba mwenge huo ili kuwataarifu mashabiki wake kile kinachoendelea.

“Kwanini mwanamuziki wa Marekani anabeba mwenge wa Uingereza? Kuna maelfu ya watu wa hapa hapa waliostahili nafasi hiyo” aliandika muingereza mmoja kwenye website ya The Sun.

Muingereza mwingine aitwaye Niamh Byrne, alitweet, “Will.i.am hana heshima kwa olympics. Kubeba mwenge huku unaandika meseji kwenye simu si jambo sahihi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents