Habari

Lady Gaga azungumzia kitendo cha kukataliwa kufanya show nchini Indonesia

Mwanamuziki wa wa pop wa nchini Marekani Lady Gaga hatimaye amevunja ukimya wake kuhusiana na kitendo cha mamlaka za nchini Indonesia kuipiga marufuku show yake mjini Jakarta.
Baada ya zaidi ya wiki ya kuwepo kwa maelezo yanayopishana na vichwa vya habari vya kimataifa kuhusu iwapo mamlaka za nchini humo zitairuhusu show yake ya June 3 mwaka huu iliyopangwa kufanyika kwenye uwanja wa Bung Karno mjini Jakarta, Gaga ametumia akaunti yake ya Twitter kutoa maelezo mafupi.
“Issue ya Jakarta ni nusu kwa nunu: Mamlaka za Indonesia zinanitaka nisifanye baadhi ya vitu kwenye show na wanaharakati wa kidini wanatishia kufanya vitendo vya ukatiliā€ aliandika jana.
“Kama show ikiwepo kama ilivyopangwa ntaimba Born This Way peke yake.”
Wiki iliyopita waziri wa masuala ya kidini nchini Indonesia Suryadharma Ali, alisema Lady Gaga hujihusisha na pornography kwa kuvaa nguo za wazi na zinazoonesha ndani kitu ambacho kingeleta picha mbaya kwa wananchi wenye umri mdogo.

Kundi la Islam Defenders Front (FPI), lilisema kuwa kwenda nchini humo kwa mwanamuziki huyo kutapeleka imani ya kishetani na kuharibu maadili ya nchi hiyo.
Zaidi ya tiketi 52,000 ambazo bei yake ni $50.75 zimeshanunuliwa kwa ajili ya concert hiyo tangu zianze kuuzwa March 10 mwaka huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents